Israel na Sudan zajadili makazi kwa Wapalestina wa Gaza
16 Agosti 2025Vyanzo hivyo vyenye ufahamu wa suala hilo lakini vilivyozungumza kwa sharti la kutotambulishwa, vimesema hakuna makubaliano yaliyofikiwa lakini mazungumzo kati ya Sudan Kusini na Israel yanaendelea.
Vyanzo hivyo vitatu vimesema matarajio ya kuwapa Wapalestinahao makazi Sudan Kusini yaliibuliwa wakati wa mikutano kati ya maafisa wa Israel na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Monday Semaya Kumba, alipofanya ziara nchini humo mwezi uliopita.
Wapalestina wana hofu juu ya Israel kujenga makazi mapya
Hata hivyo maelezo ya vyanzo hivyo yanaonekana kutofautiana na wizara ya mambo ya nje ya Sudan kusini ambayo siku ya Jumatano ilipuuzilia mbali ripoti za awali kuhusu mpango huo na kuzitaja kutokuwa na msingi.
Wizara hiyo haikuweza kufikiwa kujibu madai hayo yaliotolewa jana na vyanzo hivyo.