MigogoroMashariki ya Kati
Israel na Hamas wabadilishana mateka na wafungwa
25 Januari 2025Matangazo
Mateka hao walitambulishwa kwa majina ya Karina Ariev, Daniela Gilboa, Naama Levy na Liri Albag na walikabidhiwa kwa wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu. Israel imethibitisha kuwa mateka hao tayari wamewasili nchini humo.
Israel inatakiwa pia kuwaachilia huru wafungwa wa kipalestina wapatao 200, wakiwemo wapiganaji kadhaa wa kundi la Hamas ambao walikuwa wakitumikia vifungo vya maisha jela.
Mabadilishano haya ya mateka na wafungwa ni ya pili tangu kuanza kutekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yenye lengo la kuvimaliza kabisa vita vya miezi 15 katika Ukanda wa Gaza ambavyo vimesababisha maafa makubwa.