Israel kutuma ujumbe Doha kwa mazungumzo ya kusitisha vita
9 Machi 2025Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema imeukubali mwaliko kutoka kwa wasuluhishi.
Mazungumzo yatakayofanyika Doha yanalenga kuzishawishi Israel na kundi la Hamas kuingia kwenye awamu ya pili ya kusitisha vita inayotarajiwa kuvimaliza kabisa vita katika Ukanda wa Gaza.
Soma pia: Ujumbe wa Hamas wawasili Cairo
Makubaliano kati ya pande hizo mbili yalipata mtikisiko baada ya Israel kutaka awamu ya kwanza ya makubaliano ya usitishaji vita irefushwe huku Hamas ikitaka kuelekea moja kwa moja katika awamu ya pili kama makubaliano ya awali yanavyoainisha.
Awali wasuluhishi wa mzozo huo ambao ni Marekani, Qatar na Misri walikubaliana na kundi la Kipalestina la Hamas kusitisha vita kwa wiki sita mwezi Januari. Katika kipindi hicho, Israel iliwaachilia karibu wafungwa 2,000 wa Palestina na Hamas ikawaachilia mateka 25 walio hai.