Israel kujadili awamu inayofuata ya amani kwa Gaza
17 Februari 2025Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, imesema kuwa itaitisha mkutano wa baraza la mawaziri la usalama hii leo kujadili awamu ya pili ya mazungumzo ya amani kwa Gaza.
Ujumbe wa Israel katika mazungumzo juu ya Gaza watumwa Cairo
Ofisi hiyo imeongeza kuwa Netanyahu pia anatuma ujumbe wake mjini Cairo kuendeleza mazungumzo ya utekelezwaji wa awamu ya kwanza ya usitishaji wa mapigano Gaza.
Israel yasema itaishambulia vikali Gaza iwapo mateka wake wote hawatoachiliwa na Hamas
Ofisi hiyo pia imesema timu hiyo itapokea maagizo zaidi ya mazungumzo juu ya awamu ya pili baada ya mkutano huo wa baraza la mawaziri.
Rubio asafiri kuelekea Saudi Arabia
Baada ya ziara yake nchini Israel, Rubio amesafiri kuelekea nchini Saudi Arabia katika ziara yake ya kwanza Mashariki ya Kati kama waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Rubio asema lazima Hamas iangamizwe
Akiwa Israel, Rubio alisema kuwa kundi la Hamas haliwezi kuendelea kuhudumu kama kikosi cha kijeshi ama serikali na kwamba lazima kiangamizwe.
Akiwa kando yake, Netanyahu amesema Israelna Marekani zina mkakati wa pamoja na kwamba hali itazidi kuwa mbaya ikiwa mateka wote wa israel wanaoshikiliwa Gaza hawataachiliwa.
Ziara ya Rubio: Netanyahu asifu msimamo wa Trump kuhusu Gaza
Netanyahu pia ameongeza kuwa wamejadili kuhusu maono ya ujasiri ya Trump kwa mustakabali wa Gaza na kwamba watafanya kazi kuhakikisha kuwa yanatimia.
Matamshi hayo yanakuja siku moja baada ya Hamas kuwaachia huru mateka watatu wa Israelkwa kubadilishana na wafungwa 369 wa Kipalestina.
Iran yalaani vitisho vya Israel
Iran leo imelaani wito wa Netanyahu wa kukabiliana kabisa na kitisho chochote kutoka Iran na kuitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Netanyahu kujadili na Trump "ushindi dhidi ya Hamas" na Iran
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Israel Esmaeli Baqaei, amewaambia waandishi wa habari kwamba kutishia wengine ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa, huku akiongeza kuwa Israel haiwezi kufanya lolote dhidi ya Iran.