Israel kuimarisha usalama kwenye balozi zake duniani
22 Mei 2025Matangazo
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa amri ya kuimarishwa usalama katika balozi zote za nchi hiyo duniani baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi wafanyakazi wawili wa ubalozi wa Israel kuuwawa huko Washington Marekani.
Watu waliosikika wakidai uhuru wa Palestina walifyetuwa risasi dhidi ya wafanyakazi hao wawili wa ubalozi wa Israel, nje ya makumbusho ya kiyahudi mjini Washington Jumatano usiku.
Netanyahu amesema tukio hilo limeonesha ni kwa namna gani Israel inaandamwa na hisia za chuki na uchochezi duniani. Kansela wa Ujerumani Fredrich Merz na waziri wa mambo ya nje wa Itali Antonio Tajani ni miongoni mwa viongozi wa dunia waliolaani tukio hilo. Merz amesema tukio hilo linatisha na linapaswa kulaaniwa.