Israel imedungua kombora lililorushwa na wahouthi, Jerusalem
25 Mei 2025Matangazo
Kombora hilo lilisababisha ving'ora vya onyo la mashambulizi ya angani kusikika. Hakuna ripoti zozote hadi sasa za majeruhi au uharibifu wowote wa majengo.
Waasi hao wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wamekuwa wakiishambulia Israel kwa makombora pamoja na kulenga meli za kimataifa zinazofungamanishwa na Israel katika bahari ya shamu.
Wamesema wanafanya hivyo kupinga mashambulizi yanayofanywa na serikali ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu dhidi ya wanamgambo wa Hamas mjini Gaza.
Marekani hata hivyo iliacha kampeni yake ya kuwashambulia waasi wa Houthi mapema mwezi huu ikisma waasi hao wameahidi kuachana na mpango wao huo wa kuzishambulia meli za kimataifa katika bahari hiyo.