Israel yashinikizwa kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza
22 Julai 2025Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot ameitolea mwito hivi leo, Israel kuruhusu waandishi habari huru wa kigeni kuingia katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa na jeshi la nchi hiyo.
Wito huo umetolewa wakati tahadhari zikitolewa juu ya kuongezeka kwa janga la njaa baada ya miezi 21 ya vita.
Shirika la habari la AFP limetahadharisha kwamba maisha ya waandishi habari wa Kipalestina, wa kujitegemea wanaoshirikiana na shirika hilo ndani ya Gaza, yako hatarini na limeitolewa mwito Israel kuwaruhusu na familia zao kuondoka kwenye Ukanda huo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amesema Israel huenda ikakabiliwa na vikwazo zaidi kutoka Uingereza ikiwa haitokubali kusitisha vita Gaza.