Israel: Hamas haijabadili msimamo usitishaji mapigano Gaza
14 Machi 2025Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, imesema ingawa Israel imekubali muundo wa balozi wa Marekani kwa Mashariki ya Kati Steve Witkoff, Hamas bado inashikilia msimamo wake, na ikalishutumu kundi hilo kwa kutumia hujuma na vita hivyo vya propaganda.
Wakati huo huo, Hamas imesema leo kwamba inakusudia kumuacha huru raia mmoja mwenye uraia wa Marekani na Israel aliyetekwa nyara katika Ukanda wa Gaza.
Hamas imesema pia iiko tayari kuikabidhi wakati huo, miili ya mateka wengine wanne wenye uraia wa mataifa mawili.
Hata hivyo, kundi hilo halikutaja uraia mwingine wa Waisraeli hao wanne waliokufa.
Kundi hilo la wanamgambo limesema mpango huo umechukuliwa baada ya pendekezo lililotolewa na wasuluhishi katika mzozo huo.
Haijabainishwa wazi lini shughuli kuikabidhi miili hiyo itafanyika.