ISNTANBUL:Israel yafanya mazungumzo na Pakistan
1 Septemba 2005Matangazo
Mazungumzo ya aina yake yamefanyika kati ya Israel na Pakistan mjini Istanbul nchini Uturuki.
Mkutano huo kati ya waziri wa mambo ya nje wa Israel Silvan Shalom na mwenzake wa Pakistan Mahmood Kasuri ndio wa kwanza wa ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili kuwahi kufanyika.
Nchi hizo mbili hazina uhusiano wakibalozi lakini haijabainika iwapo mkutano huo ni wa kuanzisha uhusiano rasmi kati ya mataifa hayo.