ISLAMABAD:Misaada zaidi inakhitajiwa Pakistan
13 Oktoba 2005Matangazo
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ameiomba jumuiya ya kimataifa kutoa msaada zaidi wa pesa kushughulikia maeneo yalioathirika kwa tetemeko la ardhi.Hadi hivi sasa madola ya kimataifa yameahidi msaada wa Dola milioni 600 na pia zimepelekwa tume za misaada pamoja na helikopta na zana kama mahema,mablanketi,dawa na chakula.Rais Musharraf ametoa shukrani kwa misaada iliyotolewa hadi hivi sasa.Kwa wakati huo huo amesema kuwa itahakikishwa kwamba pesa zinazopokewa zitatumiwa kusaidia tu yale maeneo yalioathirika kwa tetemeko la ardhi.