ISLAMABAD:Kamata-kamata yaendelea nchini Pakistan
29 Julai 2005Matangazo
Vikosi vya usalama nchini Pakistan vimemkamata mtu anaetuhumiwa kuwa alishiriki katika mauaji ya mwandishi wa habari wa Kimarekani Daniel Pearl miaka mitatu ya nyuma.Hashim Qadeer anatuhumiwa kupanga mkutano kati ya Pearl na watekanyara wake.Pearl alitekwanyara mwaka 2002 alipokuwa akifanya uchunguzi wa ripoti kuhusu makundi ya wanamgambo wa Kipakistani.Baadae kilipatikana kiwiliwili chake kilichokatwa kichwa.Maafisa wa usalama wamesema Qadeer alikamatwa pamoja na wanamgambo wengine katika misako inayoendelea kuhusika na mashambulizi ya mabomu mjini London wiki tatu za nyuma.Kwa mujibu wa vikosi vya usalama katika opresheni hiyo ya msako,hadi watuhumiwa 600 wametiwa mbaroni,miongoni mwao wakiwemo pia wakuu wa kidini.