ISLAMABAD:Idadi ya vifo yafikia alfu 38 nchini Pakistan
16 Oktoba 2005Matangazo
Serikali ya Pakistan imesema inaamini kwamba watu alfu 38 wamekufa kutokana na maafa ya tetemeko la ardhi yaliyoikumba nchi hiyo wiki jana. Watu wengine alfu 60 wamejeruhiwa.
Rais Pervez Musharraf amesema anahofia , idadi ya vifo huenda ikawa kubwa zaidi.
Mashirika ya misaada pia yameeleza wasiwasi kutokana na hali mbaya ya hewa iliyosababisha kusimamishwa shughuli za uchukuzi zinazofanywa kwa helikopta.