ISLAMABAD: Watu 200 wakamatwa nchini Pakistan kuhusiana na mashambulio ya London
21 Julai 2005Matangazo
Maofisa nchini Pakistan wamewatia mbaroni watu wasiopungua 200 wanaotuhimwa kuwa wanamgambo wa kiislamu katika misako iliyofanywa nchini humo. Pakistan imekuwa ikishinikizwa kuwachukulia hatua wanamgambo wenye itikadi kali, ilipofichuka kwamba watu watatu waliojitoa muhanga kuyafanya mashambulio ya Julai saba mjini London, walikuwa waingereza wenye asili ya Pakistan.
Gazeti la Finacial Times mjini London limeripoti kwamba polisi nchini humo wanaamini makundi ya wanamgambo nchini Pakistan yatasaidia kulijibu swali ikiwa mashambulio ya London yalifanywa na magaidi hao peke yao au kwa kushirikiana na wanachama wengine wa mtandao wa kigaidi.