ISLAMABAD: Wanamgambo wa kiislamu wasakwa nchini Pakistan
20 Julai 2005Matangazo
Walinda usalama nchini Pakistan wamewakamata wanamgambo wa kiislamu katika misako inayohusiana na mashambulio ya mjini London, Uingereza. Katika matokeo ya hivi punde, wanachama wa makundi ya wanamgambo yaliyopigwa marufuku wamekamatwa katika mkoa wa Punjab.
Rais Pervez Musharaf amewaamuru polisi kupambana barabara na wanamgambo baada ya kugunduliwa kwamba watatu kati ya watu waliojitoa muhanga kuyatekeleza mashambulio ya mabomu mjini London, ni waislamu raia wa Uingereza wenye asili ya Pakistan, na walikuwa wameitembelea Pakistan mwaka jana.