Islamabad: Vikosi vya usalama nchini Pakistan vinasema...
26 Desemba 2003Matangazo
vimewatambua watu wawili waliotaka kumuuwa rais Pervez Musharaf.Watuhumiwa hao walijiripua kwa lengo la kutaka kumuuwa kiongozi wa Pakistan.Wizara ya ndani iliyotangaza habari hizo haikutoa maelezo zaidi.Jana rais Pervez Musharraf alinusurika na jaribio la kutaka kumuuwa-jaribio la pili katika kipindi cha siku kumi na moja mjini Rawalpindi,karibu na mji mkuu wa Pakistan Islamabad.Wakati huo huo rais Musharaf akizungumza kupitia televisheni ya nchi hiyo amesisitiza ataendelea kuupiga vita ugaidi.Baada ya mashambulio ya september 11 mwaka 2001 nchini Marekani rais Pervez Musharaf alijiunga na Marekani katika mapambano dhidi ya magaidi na kuchangia pia katika kung'olewa madarakani utawala wa wataliban nchini Afghanistan.