ISLAMABAD: Ulinzi wa usalama waimarishwa Pakistan
28 Julai 2007Matangazo
Hali ya usalama imeimarishwa katika mji mkuu wa Pakistan,Islamabad.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kutokea mashambulizi mawili ya kujitolea maisha muhanga.Si chini ya watu 14 waliuawa katika mashambulizi hayo,siku ya Ijumaa.Wengi waliouawa walikuwa polisi.Hapo kabla,Msikiti Mwekundu ulipofunguliwa,kulizuka mapambano makali kati ya mamia ya waumini na vikosi vya usalama. Msikiti huo sasa umefungwa tena.