Islamabad. Ujerumani yaongeza msaada wa tetemeko la aridhi.
18 Oktoba 2005Ujerumani imeongeza msaada wake katika maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi nchini Pakistan hadi kufikia Euro milioni 5.
Huduma ya misaada ya kiufundi nchini Ujerumani , THW , imetuma wafanyakazi 28 katika maeneo yaliyoathirika kusaidia juhudi za uokozi.
Huduma za utoaji misaada zimeanza tena baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na mvua kubwa na theluji.
Makundi ya waganga yanasema kuwa maelfu ya wahanga waliojeruhiwa kutokana na tetemeko hilo wanaweza kufariki iwapo msaada hautawafikia haraka.
Maafisa wa Pakistan wanasema kuwa wanahofia idadi ya watu waliofariki katika tetemeko hilo kubwa la ardhi siku 10 zilizopita inaweza kupita kiasi cha watu 54,000.