ISLAMABAD: Pakistan yapewa mikopo mipya na Japani
1 Mei 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa Japani Junichiro Koizumi,amekubali kuipa Pakistan mikopo mipya yenye thamani ya Euro milioni 120.Hatua hiyo inatazamwa kama ni juhudi ya kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili,ulio dhoofika kuhusika na masuala ya kinuklia.Tangazo la mikopo hiyo limetolewa licha ya Tokyo kuwa na wasi wasi wa utapakaaji wa silaha za nyuklia akihusika mwanasayansi mkuu wa Pakistan.Japani ikiwa ni nchi pekee iliyoathirika kwa shambulio la kinyuklia,inataka ipewe maelezo ya uchunguzi uliofanywa kuhusu kashfa iliyochomoza hadhrani mwaka uliopita.Kabla ya kwenda Pakistan,waziri mkuu Koizumi alikuwa na ziara ya siku mbili nchini India ambako aliahidi kuboresha uhusiano katika sekta za uchumi na usalama.