Islamabad. Pakistan kuahirisha ununuzi wa ndege za kivita.
5 Novemba 2005Rais wa Pakistan Pervez Musharaff amesema kuwa ataahirisha ununuzi wa ndege za kivita kutoka Marekani ili kupata fedha za kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi.
Ripoti za vyombo vya habari zimesema kuwa Pakistan ilikuwa inunue ndege 25 za kivita aina ya F-16 kutoka Marekani , kwa thamani ya dola milioni 25 kila moja.
Fedha zinazohitajika kwa ajili ya utoaji misaada ya watu walioathirika na tetemeko la ardhi zinakadiriwa kufikia dola bilioni 5.
Kiasi cha watu milioni tatu hawana mahali pa kuishi mwezi mmoja baada ya tetemeko hilo lililoharibu sehemu kubwa ya jimbo la Kashmir nchini Pakistan.
Umoja wa mataifa unasema kuwa umepokea kiasi kidogo tu cha fedha za misaada zilizoahidiwa na jumuiya ya kimataifa.