ISLAMABAD: Mahema zaidi yahitajiwa nchini Pakistan
19 Oktoba 2005Matangazo
Siku 11 baada ya kutokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Pakistan,takriban watu nusu milioni walionusurika katika vijiji vilivyo mbali,wangali wakingojea kupokea misaada.Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshghulikia Mipango ya Chakula Duniani-WHO.Shirika hilo limeongezea kuwa kuna khofu kwamba itakuwa vigumu kuzuia maafa zaidi huku majira ya baridi yakikaribia.Ripoti zinasema kuna watu waliofariki kwa sababu ya baridi kali.Kwa mujibu wa serikali ya Pakistan,idadi ya vifo huenda ikafikia 53,000.Kiasi ya watu milioni 3 hawana mahala pa kuishi na Umoja wa Mataifa unasema majira ya baridi kali yakijongea,bado kuna upungufu mkubwa sana wa mahema ya kuwapa joto.