ISLAMABAD: Jeribio la kombora nchini Pakistan
19 Machi 2005Matangazo
Pakistan kwa mafanikio imefanya jeribio la kombora lenye uwezo wa kubeba silaha ya kinuklia.Kwa mujibu wa maafisa wa kijeshi kombora hilo chapa ya Shaheen namba II,linaweza kuchukua aina zote za silaha za kawaida na vichwa vya kinuklia umbali wa hadi kilomita 2,000.India na nchi nyingi zingine katika eneo hilo ziliarifiwa hapo kuhusu jeribio hilo.Rais Pervez Musharraf alieshuhudia jeribio hilo amesema,Pakistan haitohifadhi tu uwezo wa miradi yake ya kinuklia na makombora bali itajitahidi pia kuiboresha miradi hiyo.