ISLAMABAD: Jan Egeland azuru Pakistan
13 Oktoba 2005Matangazo
Kiongozi wa shirika la kutoa misaada la umoja wa mataifa, Jan Egeland, amesema manusura wa tetemeko la ardhi nchini Pakistan wanahitaji misaada ya dharura huku wengi wao wakiwa bado hawawezi kufikiwa siku tano baada ya tetemeko la Jumamosi iliyopita. Egeland amesema ipo haja ya kupeleka helikopta zaidi, maji safi ya kunywa, mahema na fedha kuwasaidia waathiriwa.
Alipokuwa akirudi mjini Islamabad kutoka Muzaffarad, Egeland aliwabeba watoto watatu wanaohitaji matibabu baada ya kujeruhiwa katika tetemeko hilo. Amekanusha madai ya wakaazi wa eneo hilo walioachwa bila makao na wanaokabiliwa na njaa, kwamba msaada wa umoja wa mataifa unachelewa kuwafikia.