Islamabad: Idara ya usalama ya Pakistan imezitambua maiti ...
26 Desemba 2003za wanaharakati waliotaka kumuuwa rais Pervez Musharaf hapo jana mjini Rawalpindi.Habari hizo zimetangazwa na waziri wa mambo ya ndani Faisal Saleh Hayat.Vyombo vya habari vimemnukulu waziri Hayat akisema watu waliohusika na njama ya kutaka kumuuwa rais Musharaf wamegunduliwa.Jeneral Pervez Musharaf alinusurika chupu chupu jana katika shambulio la kutaka kumuuwa.Magari mawili ya serikali yaliyokua nyuma yake yameripuliwa , watu 14 wameuwawa na wengine 46 kujeruhiwa.Hii ni mara ya pili katika kipindi cha siku 11,kwa rais Pervez Musharak kunusurika na njama ya kutaka kumuuwa .Kiongozi huyo wa Pakistan anahisi njama hizo zimeandaliwa na "magaidi na wafuasi wa itikadi kali wanaopinga mchango wa Pakistan katika opereshini zinazoongozwa na Marekani dhidi ya ugaidi."