Iraq yamkamata mshukiwa wa IS kwa shambulizi la New Orleans
27 Aprili 2025Matangazo
Baraza Kuu la Mahakama la Iraq limesema kuwa mwanachama huyo wa IS alikamatwa baada ya nchi hiyo kupokea ombi kutoka Marekani kusaidia katika uchunguzi.
Pia limeongeza kuwa mshukiwa huyo ni mwanachama wa ofisi ya operesheni za nje ya kundi la kigaidi la IS.
Mshambuliaji wa New Orleans alichochewa na IS
Baraza hilo limesema kuwa mshukiwa huyo atahukumiwa nchini Iraq chini ya sheria ya kupambana na ugaidi.
Mji katika jimbo la kusini la Louisiana uliingiwa na hofu mapema siku ya mwaka mpya wakati mwanajeshi mkongwe wa jeshi la Marekani,ambaye shirika la ujasusi la FBI lilieleza alikuwa na mafungamano na IS, alipovurumisha lori katikati ya watu.