Iraq kusamehewa madeni yake:
17 Desemba 2003Matangazo
BERLIN: Kama vile Ufaransa, nayo Ujerumani itayari kuisamehe Iraq sehemu kubwa ya madeni yake, aliarifu msemaji wa serikali Bela Anda baada ya kumalizika mazungumzo kati ya mjumbe maalumu wa Marekani James Baker na Kansela Gerhard Schröder. Kusuluhishwa tatizo la madeni ya Iraq ni muhimu sana kwa ukarabati wa kiuchumi wa nchi hiyo, alisema msemaji huyo wa serikali ya Berlin. Muundo wa msamaha huo wa madeni ya Iraq utazidi kujadiliwa katika mkutano wa lile kundi Kilabu ya Paris la mataifa fadhili, aliendelea kusema. Imetathminiwa hivi karibuni kuwa Iraq inadaiwa jumla ya Dollar Biliyoni 120 na mataifa ya kigeni. - Mjini Washington, serikali ya Marekani imekaribisha maamuzi ya Ufaransa na Ujerumani ya kuisamehe Iraq madeni yake.