IRAQ IPUNGUZIWE MADENI
29 Desemba 2003Matangazo
BEIJING: Mjumbe maalum wa Marekani nchini Iraq yupo Jamhuri ya Watu wa Uchina akijaribu kuishawishi serikali ya Beijing kuisamehe Iraq madeni yake.Hapo awali Ujapani ilisema kuwa ipo tayari kuisamehe Iraq sehemu kubwa ya madeni yake.Wizara ya kigeni ikitangaza habari hizo imeeleza kuwa Ujapani itasamehe sehemu ya deni la Iraq ikiwa madola mengine 19 ya "Paris Club"ambayo ni wakopeshaji,yatafanya hivyo pia.Kwa hivi sasa Iraq inadaiwa na Ujapani zaidi ya Euro bilioni 3.James Baker ametoa muito kwa nchi fulani za bara Asia kupunguza madeni ya Iraq.Baker katika maombi yake ya kutaka Iraq ipinguziwe madeni,ameshafanikiwa Berlin,Paris, Roma,London na Moscow.