Iran yawanyonga wanamgambo 9 wa Dola la Kiislamu, IS
10 Juni 2025Matangazo
Shirika la habari la idara ya mahakama ya Iran la Mizan limetangaza kunyongwa kwa wanamgambo hao likidai kuwa hukumu hiyo ya kifo ilikuwa imeidhinishwa na mahakama ya juu nchini humo.
Shirika hilo la habari la Mizan limesema wanamgambo hao walikamatwa wakati wlaipokuwa katika mapambano na Jeshi la Mapinduzi la Iran, ambapo wanajeshi watatu waliuwawa pamoja na wapiganaji kadhaa wa kundi la Dola la Kiislamu.
Kundi la itikadi kali la Dola la Kiislamu ambalo wakati mmoja lilikuwa linadhibiti sehemu kubwa ya Irak na Syria, lilishambuliwa na kumalizwa nguvu na Marekani mwaka 2014.
Kundi hilo limesambaratika kutoka wakati huo ingawa limekuwa likifanya mashambulizi kadhaa makuu.