Iran yawanyonga kiasi watu 975 mwaka jana
20 Februari 2025Matangazo
Shirika la haki za binadamu la Kiiran, lenye makao yake Norway, IHR na ECPM la Ufaransa linalopinga adhabu ya kifo, kwa pamoja yamesema, idadi hiyo ya waliohukumiwa kifo na kunyongwa nchini Iran ndio kubwa zaidi kuonekana nchini humo tangu mwaka 2008.
Mashirika hayo yameishutumu Iran kwa kutumia adhabu ya kifo kama silaha kubwa ya kufanya ukandamizaji wa kisiasa.
Soma pia:Iran yaashiria kuwa tayari kuzungumza na Trump licha msimamo wake mkali
Mkurugenzi wa IHR Mahmood Amiry Moghaddam, amesema utekelezaji huu wa adhabu ya kifo, uliofanywa na utawala wa Iran, ni vita dhidi ya umma wake ili kuendelea kubakia madarakani.