Iran yathibitisha kurejea kwenye meza ya mazungumzo
21 Julai 2025Iran imethibitisha itafanya mazungumzo na Ujerumani Ufaransa na Uingereza Ijumaa wiki hii mjini Istanbul kuhusu mpango wake wa nyuklia. Mazungumzo hayo yatakuwa ya kwanza tangu Marekani ilipoviishambulia vinu vya nyuklia vya Iran mwezi mmoja uliopita.
Wanadiplomasia wa Iran watakutana na wenzao wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani, nchi zinazofahamika kama E3, baada ya nchi hizo tatu kuonya kwamba vikwazo huenda vikawekwa tena dhidi ya Iran iwapo haitarejea katika meza ya mazungumzo kuhusiana na mpango wake wa nyuklia.
Televisheni ya kitafia ya Iran imemnukuu msemaji wa wizara ya mambo ya nje, Esmail Baghai Jumatau akisema kwa kujibu ombi la nchi za Ulaya, Iran imekubali kufanya duru mpya ya mazungumzo.
Mwanadiplomasi wa Ujerumani amesema nchi za E3 zinawasiliana na Iran na nchi hiyo haitakiwi kabisa kuruhusiwa kutengeneza silaha za nykulia.