Iran: Tunayo haki ya kurutubisha madini ya Urani
3 Mei 2025Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, Abbas Araghchi kupitia ukurasa wake wa X amesema Iran ina kila haki ya kumiliki kikamilifu nishati ya nyuklia akitolea mfano nchi yake kuwa ni moja ya mataifa yaliyotia saini Mkataba wa Kuzuia kusambaa kwa silaha za nyuklia (NPT).
Soma zaidi: Iran yaishutumu Israel kwa kudhibiti sera ya Marekani kwenye mazungumzo ya nyuklia
Aragchi amesema kuna mataifa kadhaa yaliyotia saini mkataba huo ambayo yanarutubisha madini ya urani lakini yanazipinga silaha hizo. Chini ya mkataba huo nchi wanachama zinalazimika kutaja hifadhi zao za nyuklia na kuziweka chini ya usimamizi wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IEA.